Menu
Home
Trending
Popular
Favorites

Jinsi ya Kupata Hati ya Mshahara (Salary Slip)

Ili kupata hati ya mshahara kwa njia ya mtandao, unaweza kujisajili kwenye portal

May 28, 2025

Jinsi ya Kupata Hati ya Mshahara (Salary Slip)

Ili kupata Hati ya Mshahara unatakiwa kujisajili kwenye mfumo wa Watumishi Portal. Kwenye mfumo huu wa watumishi utakuwezesha kupata taarifa zako za kiutumishi.

Vitu vya kuzingatia:

  • Fahamu Majina yako kamili

  • Hakikisha una barua pepe kama huna utalazimika kufungua

  • Fahamu CHECK NO namba yako

Ili kujisajili Bofya hapa Kujisajili kwenye mfumo


Pia unaweza kupata hati yako ya mshahara kwa kutumia mfumo mpya wa "Government Salary Slip Portal" ambapo utajisajili kwenye mfumo.

Kwenye Mfumo huu vitu vya kuzingatia ni:

  • Check namba ya mtumishi

  • Majina kamili kama yalivyo kwenye mfumo wa Rasilimali Watu yaani HCMIS maarufu kama Lawson.

  • Tarehe ya kuzaliwa.

  • Vote Code, Sub Vote Code, Namba ya Akaunti ya Benki unayopitishia mshahara.

  • Fahamu pia Salary Scale, Salary Grade na Salary Step.

  • Barua pepe (Email) inayofanya kazi.

Ili kujisajili Bofya  https://salaryslip.mof.go.tz/Manage/EmployeeRegistration au kuingia kwa waliojisajili kwenye Government Salary Slip Portal Bofya  https://salaryslip.mof.go.tz/Account/Login?ReturnUrl=%2F

Share this article:

User Comments (0)

No comments yet